Tuesday, January 16, 2018


Timu Ya Taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys itaendelea kuwepo kambini mpaka Januari 28, 2018.
Maandalizi hayo ya Serengeti Boys yatakwenda sambamba na kucheza mechi za kirafiki kabla ya kuaihirisha kambi hiyo itakayokuwa ikifanyika mara kwa mara na mpango uliopo ni kila mwezi timu hiyo kuingia kambini.
Katika hatua nyingine kikosi hicho kimepunguzwa kutoka wachezaji 43 walioitwa mpaka kufikia 34 watakaoendelea na kambi hiyo.
Orodha hiyo inajumuisha wachezaji 30 wa ndani na magolikipa wanne.

0 comments:

Post a Comment