Manchester City wameamua kuacha kutafuta mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.
Taarifa
zinasema klabu hiyo imeamua kufanya hivyo baada ya kuwa itakuwa ghali
sana kuendelea kutaka kumnunua mchezaji huyo raia wa Chile mwenye miaka
29.Meneja Pep Guardiola, mmiliki wa klabu hiyo Khaldoon al Mubarak na maafisa wengine wakuu wa klabu hiyo wote wamekubaliana na msimamo huo.
Inaarifiwa kwamba ujira anaotaka Sanchez utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi miongoni mwa wachezaji wa City iwapo atahamia klabu hiyo.
Hili ni jambo ambalo klabu hiyo haiko tayari kufanya.
Manchester United sasa wana nafasi nzuri ya kumnunua mchezaji huyo baada ya kudokeza kwamba wako tayari kulipa £35m ambazo Gunners wamekuwa wakitaka kulipwa.
Duru zinasema kwamba Chelsea pia wameanza kumnyatia mchezaji huyo.
Taarifa zinasema gharama kamili ya uhamisho wa Sanchez ambayo inajadiliwa ni zaidi ya £60m ambazo Arsneal walikuwa wamekubali kuwauzia City majira ya joto yaliyopita.
City bado wanaamini Sanchez angelipenda kujiunga nao, ikizingatiwa kwamba amewahi kucheza chini ya Guardiola zamani, wakiwa Barcelona.
Aidha, Sanchez mwenyewe ndiye aliyekuwa akishinikiza kuhama kwake Agosti.
Hata hivyo, wanaamini uwezekano wa Sanchez kushusha madai yake ya mshahara hadi kiwango ambacho watamudu ni finyu.
Akizungumza baada ya ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Stoke Jumatatu, meneja wa United Jose Mourinho alisema: "Hakuna taarifa zozote mpya kumhusu Sanchez. Bado ni mchezaji wa Arsenal; akisalia Arsenal, vyema wka Arsena, akija kwetu, vyema kwetu, akihamia klabu nyingine, vyema kao.
"Huenda pengine kuna klabu nyingine zinazomtaka na zinajaribu na sifai kuzungumzia mchezaji ambaye bado yuko Arsenal.
"Sina imani lakini sijakosa imani sana. Akichukua hatua, nafikiri tutakuwa na nafasi."
0 comments:
Post a Comment