United wanaweza fanya kile cha 1995/1996 na kubeba EPL msimu huu
Msimu wa soka EPL mwaka 1995/1996 wakati kama huu klabu ya Newcstle ilikuwa ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama 12 (kama Man City) na United walikuwa nafasi ya 3 lakini ligi ikaisha United wakiwa mabingwa.
Katika wakati huo tayari michezo 23 ilikuwa imechezwa huku Newcastle akiwa na alama 54, Liverpool wakifuatia wakiwa na alama 42 na United nafasi ya 3 na alama 42 lakini mwisho wa msimu United alimaliza na alama 82 huku Newcastle akimaliza na 78.
Hapo jana United wamepata alama 3 na sasa wako nyuma ya City kwa alama 12, Antonio Valencia alifunga bao la kwanza kwa mguu wa kushoto na hii ikiwa mara yake ya kwanza kufunga kwa mguu wa kushoto tangu 2007/2008.
Paul Pogba alitoa assist ya bao la pili la Anthony Martial ambapo hii inakuwa assist yake ya 9 msimu huu na hakuna mchezaji yoyote EPL mwenye assist nyingi kumzidi Paul Pogba na huku nafasi 4 kati ya 7 alizotengeneza EPL zimezaa mabao.
Romelu Lukaku michezo yake mitatu iliyopita hakuwa na shot on target na hiyo ilikuwa mara ya kwanza ndani ya miaka 2 lakini usiku wa jana alifanikiwa kupiga mashuti 3 langoni kwa Stoke City huku moja likizaa matunda.
0 comments:
Post a Comment