Liverpool wana nia ya kumsaini Riyad Mahrez huku
mshambuliaji huyo wa Leicester City raia wa Algeria akitarajiwa
kufanyiwa uchunguzi wa kiafya leo Jumapili. (Bein Sports)
Liverpool
wako tayari kufanya hima kujaza pengo lilioachwa na Philippe Coutinho
ambaye ameelekea Barcelona huku wing'a wa Monaco Thomas Lemar 22, akiwa
nambari moja katika orodha yao.
Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa ya paunia
milioni 25 kwa mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, lakini hatua
hatua hiyo itafikisha kikomo mbio za kumtafuta mlinzi wa Real Sociedad,
Inigo Martinez. (Sunday Mirror)
Ciy pia wanamwinda mlinzi wa
Leicester Harry Maguire, 24, na wanaweza kutoa ofa ya pauni milioni 50
kwa kiungo huyo wa kati wa zamani wa Hull City. (Sun on Sunday)
Manchester
United huenda wakajaribu kumleta Gareth Bale kutoka Real Madrid, kabla
ya msimu wa kununua wachezaji wapya kukamilika. (Sunday Express)
Arsenal wanakabiria kuafikia makubalianoa ya pauni
milioni 25 kwa kiungo wa kati wa West Brom raia wa Ireland Kaskazini
Jonny Evans, 30. (Sun on Sunday)
Meneja Mauricio Pellegrino anasema Southampton wana matumaini ta kumsaini wing'a wa Arsenal na England Theo Walcott, 28. (ESPN)
Meneja
wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amekana madai ya kumuuza kiungo wa kati
raia wa Chile Arturo Vidal kwenda Chelsea mwezi Januari (Mail on
Sunday)
Home
»
»Unlabelled
» Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 07.01.2018
Sunday, January 7, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment