Sunday, January 7, 2018


YANGA SC wanacheza mechi yao ya nne ya Kundi B Kombe la Mapinduzi leo watakapomenyana na Zimamoto Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia 10:30 jioni.
Yanga wanataka kuendeleza wimbi la ushindi japokuwa wamekwishafuzu Nusu Fainali, ili kujiwekea mazingira ya kuongoza kundi lake dhidi ya vinara wa sasa, Singida United wenye pointi 12 baada ya mechi zao nne.
Ikumbukwe Singida  na watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na Yanga SC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tisa Jumatatu. 
Wachezaji wa Yanga, Amissi Tambwe na Hassan Kessy wakiwa mazoezini
Kwa ujumla mechi za makundi zitahitimishwa Januari 8, kwa mchezo kati ya Simba SC na URA ya Uganda Saa 10:30 jioni Yanga SC dhidi ya  Singida United  Saa 2.1530 jioni.
Januari 9 itakuwa ni mapumziko kabla ya Nusu Fainali kuchukua nafasi Januari 10 kwa mechi kati ya Mshindi wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Mshindi wa Pili Kundi B Saa 10:30 jioni na Mshindi wa kwanza wa Kundi B dhidi ya Mshindi wa Pili Kundi A, wakati fainali itafuatai Saa 2:15 usiku Januari 13.

0 comments:

Post a Comment