Saturday, January 20, 2018



Hamid Mbwezeleni Mwenyekiti kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF
Kamati ya maadili ya TFF imetoa hukumu leo Ijumaa Januari 19, 2018 kwa viongozi wa nne wa soka waliokuwa wakituhumiwa kwa kughushi na udanganyifu wa mapato ya mchezo wa ligi kuu kati ya Ndanda FC dhidi ya Simba uliochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara Disemba 30, 2017.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Hamid Mbwezeleni ametangaza kumfungia Dustan Mkundi kutojihusisha maisha na masuala ya soka, Mkundi alikuwa ni msimamizi wa kituo cha Mtwara.
Kamati hiyo pia imemfungia Kizito Mbano kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitano, Mbano alikuwa ni Katibu Mkuu wa chama cha soka mkoa wa Mtwara.
Selemani Kachele ambaye ni Katibu msaidizi wa klabu ya Ndanda amepewa onyo kali huku mhasibu wa Simba Selemani Kahumbu akiondelewa tuhuma dhidi yake.
Kamati hiyo imesema, watuhumiwa hao walishtakiwa mbele ya kamati kwa tuhuma za kughushi kwamba mapato ya mchezo wa Ndanda vs Simba yalikuwa ni zaidi ya Tsh. 34,000,000 lakini ilithibitika mapato katika mechi hiyo yalikuwa ni zaidi ya Tsh. 37,000,000.

0 comments:

Post a Comment