MSHAMBULIAJI
wa zamani wa Swansea, Bafetimbi Gomis jana alizimia uwanjani wakati wa
mechi kati ya timu yake ya sasa, Galatasaray dhidi ya wenyeji Kasimpasa
walioshinda 2-1 katika Ligi ya Uturuki.
Gomis alipoteza fahamu, lakini akaruhusiwa kuendelea na mchezo baada ya kuzinduka.
Tukio
hilo lilitokea dakika ya saba ya mchezo, baada ya Gomis kuinama kushika
magoti yake kabla ya kuanguka uwanjani na kuzimia huku wachezaji
wenzake wakimzinguka kwenye eneo la kona ya Galatasaray.
Mwaka
2009 Gomis aligundulika kuwa na presha ya kushuka kiasi cha kuzimia.
Mwaka huo, alizimia kwenya kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa
na akazimia tena katika matukio mengine matatu.
Mshambuliaji wa Galatasaray, Bafetimbi Gomis jana alizimia uwanjani katika mechi dhidi ya Kasimpasa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kwa siku za karibuni, Gomis alizimia tena wakati bado anacheza Swansea katika mechi dhidi ya Tottenham mwaka 2015.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 32 anaweza kupoteza fahamu kwa muda, lakini
kupatiwa huduma ya kwanza anaweza kuzinduka na kuendelea kucheza.
Gomis amefunga mabao 20 kwenye mechi 26 alizoichezea Galatasaray kwenye mashindano yote tangu ajiunge nayo msimu uliopita.
Baada
ya kujiunga na Swansea kutoka Marseille mwaka 2014, Gomis alifunga
mabao 17 katika mechi 71 za mashindano yote za klabu huyo ya Wales.
0 comments:
Post a Comment