Kuna mambo ya ajabu huwa yamewahi kutokea sana kwenye michuano ya UEFA. Ifuatayo ni orodha ya mechi zilizowaacha mashabiki midomo wazi.
Barcelona 0-4 Dynamo Kiev
Mwaka 1986 wazazi wa Andriy Shevchenko ilibidi wamkimbize sheva kutoka wilaya ya Minsk kukwepa bomu la Chernobyl liliopigwa pale. Huenda bomu lingehatarisha kabisa maisha yake. Kwa bahati nzuri wazazi wake walimuondoa mapema. Mbaya zaidi walimuokoa muuaji wa Barcelona miaka 11 baadae. Sheva alipiga Hatrick katika mchezo wa Kwanza Mjini Kiev Barcelona akifa 3 kwa Nungr. Mbele ya Rivaldo, Luis Figo, Xavi, Patrick Kluivert, Frank De Boer, Luis Garcia, na Oscar wote hawa hawakufua dafu. Mabingwa hawa wa La Liga walitandikwa goli 3 bila majibu na iliwashangaza wengi. Rafiki yake Sheva alimwambia Sheva umeotea tu, Sheva alicheka sana. Rafiki yake akamwambia mkienda Camp Nou hutoki. Camp Nou nako Barcelona hakuonewa aibu pia alitandikwa Vinne.
Barcelona 3-1 Manchester United
Ishu kubwa hapa sio matokeo haya, ishu inakuja inakuwaje unaifunga Man United tena ndani ya ardhi yao? Sio kwamba kocha ni Moyes au Van Gaal. Noooo… kocha Sir Alex Ferguson… daah ndugu yangu.. Ferguson mwenyewe anakiri katika maisha yake hakuwahi kukutana na timu ngumu kama ya Guardiola. Na kituko kikubwa ni pale Fergie aliposhindwa kutafuna bablishi kwa meno akaanza kutafuna na mikono (vidole vilitetema kwa hofu) sio kwa mpira ule.
Monaco 3-1 Real Madrid
Ukimuuliza Carlos Queiroz kocha mkuu wa Real Madrid kuwa kilichotokea nini mwenyewe hajui. Mchezo wa kwanza waliishindilia Monaco Magoli 4-2. Kimahesabu tunasema mchumba ameshang’ata kucha tayari. Lakini Kibiashara tunasema kama muajiriwa wako wa zamani amekutoa kwa mkopo na anakulipa mshara kwa zaidi ya asilimia 65 kimsingi hupaswi kushangilia ukiona na ashindwa. Fernando Morientes nadhani hii prinsipo yeye haijui. Alichokifanya baada ya kushindilia goli kwenye mchezo wa marudiano yeye alishangilia licha ya kwamba alikuwa ametokea kwa mkopo Real Madrid. Monaco walikuwa chini magoli 4-2 lakini Morientes akabdilisha matokeo na kuwa 3-1. Madrid walibutwaa maana ndani walikuwa na Ronaldo De lima, Raul, na Zinedine Zidane. Morientes alitumia dakika 45 za mwisho kupeleka kilio kwa waliomkataa. Madrid wakaondoshwa kwa Magoli 5-4.
Deportivo la Coruna Vs Ac Milan
Mchezo wa kwanza Ac Milani walishinda magoli 4-1. Magoli ya Walter Pandiani, Juan Carlos ValerĂ³n, Alberto Luque na Fran yalimpa kiburi Carlo Ancellot kutoka san Siro kifua wazi. Waliposafiri kwenda Nchini Hispania, La Coruna walipata goli la kwanza kupitia, Juan Valerin akaweka kingine dakika ya 35, Albert Luque akafunga mahesabu dakika za mwisho kipindi cha kwanza. Ancellot alichanganyikiwa sana kipindi cha pili, akamtoa Tomasson, na Pirlo akawaleta Rui Costa na Inzaghi ambao waliachwa benchi kwa kuamini kuwa kazi iliisha San Siro. Hilo halikusaidia maana Fran aliingia kipindi cha pili na dakika 66 akakamilisha goli la 4 na Ac Milan kuondolewa.
Barcelona 6-1 PSG
Hebu jaribu kufumba macho halafu fikiria kile kilichotokea dakika 90 Pale Ufaransa halafu fananisha na kile ulichokiona Camp Nou. Au fikiria mtu yeyote aliyeaga dunia baada ya Barcelona kupata kipigo cha magoli 4 kwa bila halafu afufuke leo umwambie ile mechi Barca alishinda 6. Ukiwa na lionel Messi kila kitu kinawezekana lakini kwa lile Yule malaika wa Michezo aliyekuwa zamu ile siku atuambie ilikuwaje.
MILAN vs LIVERPOOL
Kama kuna kitu ambacho mashabiki wa Liverpool walichobaki nacho akilini mwao ni ile kam baki yao kule Instunbul. Huwezi kuandika historia yoyote ya UEFA hili tukio usiliweke. Mtu anapigwa 3 kipindi cha kwanza kipindi cha pili anachomoa zote na anakwenda kushinda kwenye matuta? Benitez kuna kizizi alitumia si bure.
0 comments:
Post a Comment