Tuesday, March 6, 2018


Wawakilishi wa Tanzania Bara wa michuano ya klabu bingwa Barani Afrika klabu ya Yanga hii leo wamekubali kipigo cha mabao 2 – 1 kutoka kwa timu ya Botswana ya Township Rollers FC mchezo uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tshireletso kutoka timu ya Township Rollers FC kisha Obrey Chirwa akaisawazishia Yanga SC  kabla wa Botswana hawajahitimisha karamu ya mabao kwa kupitia mchezaji wao Motsholetsi Sikele na kuufanya kumalizika kwa matokeo hayo ya mabao 2 – 1.
Yanga SC inatarajia kurejea tena kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano wiki moja ijayo huko nchini Botswana na kutarajiwa kuwa na kibarua kizito cha kuhakikisha wana chomoza na ushindi wa mabao 3 – 0 ugenini ili kujihakikishia kusonga mbele.
Wawakilishi wengine wa kimataifa timu ya Simba inatarajia kushuka dimbani hapo kesho siku ya Jumatano kuivaa Al- Masry katika kombe la Shirikisho Barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment