Wednesday, March 7, 2018


Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 51 katika ushindi wa 2-1 usiku wa Jumanne dhidi ya wenyeji, Paris Saint Germain kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Bao la pili lilifungwa na Carlos Henrique Casimiro dakika ya 80, baada ya Edinson Cavani kuisawazishia PSG dakika ya 71 na sasa kikosi cha kocha Zinedine Zidane kinakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada ya awali kushinda 3-1 mjini Madrid. PSG ilimaliza pungufu baada ya kiungo wake, Marco Verratti kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 66 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

0 comments:

Post a Comment