Monday, March 19, 2018

Louis Van Gaal aibuka tena na kuwashambulia United

540
0
SHARE
Bado anaonekana kama ana kinyongo ndani yake, kocha wa zamani wa Manchester United Louis Van Gaal anaendelea kuizungumzia Manchester United lakini amekuwa akiizungumzia kwa mabaya.
Safari hii LVG ameibuka na kusema kwamba wachezaji wengi wa Manchester United sio weledi na walikuwa kama hawajui wanachofanya ndio sababu ya yeye kukwama United.
Van Gaal anasema alijaribu kutafuta namna ya kuwaliana na wachezaji wake, kupitia mtaalamu wake wa IT walitengeneza namna ambayo wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepe mtandaoni (email).
Cha kushangaza ni kwamba pamoja na Van Gaal kujitahidi kutafuta mbinu hiyo ili kujiweka karibu na wachezaji wake lakini waliipotezea na hawakuwa wakisoma hata hizo email ambazo alikuwa akituma.
Van Gaal anasema aina hiyo ya mawasiliano aliifanya pia akiwa Bayern Munich na wachezaji walikuwa wakisoma email zake, Unites walikuwa wanasema wamezisoma lakini haikuwa kweli.
LVG pia amezungumzia jaribio lake la kumnasa mshambuliaji wa Bayern Munich Roberto Lewandoski ambapo amesema Unites walikuwa tayari kutoa kiasi chochote kile cha pesa lakini Bayern waliwawekea ngumu.

0 comments:

Post a Comment