Carvalhal ameachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kufikia mwisho ikiwa ni miezi mitano imepita tangu alipotangazwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akitokea Sheffield Wednesday.
Swansea nao wamethibitisha tukio hilokupitia mtandao wao wa Twitter kwa kuandika, “We can confirm that the club will not be extending Carlos Carvalhal’s contract. Everyone at the #Swans would like to thank Carlos for his efforts and wish him all the best for the future.”
Inadaiwa kuwa sababu ya kocha huyo kushindwa kuongeza mkataba mpya ni kutokana na kushuka daraja baada ya kushika nafasi ya 18 kwenye ligi kuu wakiambatana na Stoke City pamoja na West Bromwich Albion.
Kwa sasa Swansea watalazimika kumtafuta kocha wa tano kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha miezi 19.
0 comments:
Post a Comment