WASHAMBULIAJI wanaocheza Ligi Kuu ya England, Anthony Martial na Alexandre Lacazette wote wametemwa kwenye kikosi cha Ufaransa kuelekea Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao.
Kocha
Didier Deschamps amewaingiza wachezaji wote hao kwenye kikosi cha
wachezaji wa akiba, kama itatokea kati ya aliowateua watapata tatizo
atawageukia Martial na Lacazette.
Mshambuliaji
wa Chelsea, Olivier Giroud amebahatika kuingia kwenye orodha ya mwisho
ya wachezaji 23 pamoja na Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Nabil Fekir,
Thomas Lemar, Antoine Griezmann na Florian Thauvin.
Kikosi kamili cha Ufaransa cha Kombe la Dunia katika picha iliyothibitishwa kwenye Twitter jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment