Monday, May 28, 2018


ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU 17 KUELEKEA RUSSIA TUZIKUMBUKE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2002 NA KIZAZI CHA DHAHABU CHA TIMU YA URENO NA MECHI YAO DHIDI YA MAREKANI. Na Elizabeth Lyuvale
Ikiwa ni Mara ya kwanza Kwa fainali hizi za 17 za Kombe la dunia kufanyika bara la Asia na nchi mbili kuwa mwenyeji Japan na Korea kusini pia ikawa Mara ya mwisho Kwa sheria ya Golden Goal kutumika.
Tmu ya taifa ya ureno katika kiwango bora na wachezaji nyota duniani, ilipangwa kundi moja na timu za Marekani, Poland na mwenyeji Korea kusini.

Kwa kuangalia kundi hili wareno hawa walipewa asilimia kubwa kuvuka kwenda hatua inayofuata na timu nyingine walizopangwa nazo zilikua under dogs yani zilipewa asilimia ndogo mno yakumfunga mreno.

Mwaka huo Wa 2002 ureno ilikua na kizazi bora tena cha dhahabu huku wakiongozwa na uwepo Wa mchezaji bora Wa dunia kwa mwaka huo Luis Figo na wakali kibao kama kiungo mshambuliji wao mahiri Rui Costa, mfungaji Joao Pinto na ulinzi ulotukuka wa Jorge Costa.
Tena kukiwa na chipukizi hodari Cristiano Ronaldo japo alikua akisumbuliwa na goti kipindi hicho waliingia katika mashindano.

Hakika walikwenda Asia wakiwa na imani yakufika mbali. Mechi yao ya kwanza dhidi ya marekani iliduwaza wapenzi wengi wa soka.
Mechi ilianza kwa kasi. Marekani dakika ya nne tu wakapata goli kupitia kwa John O’Brien, huku wareno wakipambana kuchomoa bao hilo.

Landon Donovan akaiongezea timu yake ya Marekani goli la pili. Safari hii mpira ukamgonga beki wa Ureno Jorge Costa dk ya 29 nakujaa kambani. Hata hivyo waswahili husema mlamba asali haachi, wamarekani walizidi kulisakama lango la wareno.

Vijana wa George Bush zamu hii Brian McBride akawaandikia marekani bao la tatu dk ya 36 hivyo ndani ya dk ya 37 za mchezo ubao ukawa unasoma marekani 3 na ureno 0.

Wareno walifanikiwa kupata bao moja kabla ya kipindi cha kwanza kuisha dk ya 39 kupitia kwa Beto Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza. Zikiwa zimesalia dk 20 mpira kumalizika beki Agoos dk ya 71 akajifunga na kuwarudisha warenk mchezo wakiwajua fika kwamba wana deni la goli moja.

La kuvunda halina ubani, Zamu hii miti yote iliteleza, sio Figo wala Ini kilichoweza kubadili matokeo. Mtanange ukamaliza kwa mabao 3-2.

Kikosi cha Ureno, Victor baia golini,
Mabeki : Beto, Rui Jorge, Fernando couto na Jorge Costa
Viungo: Sergio conceicao, Rui Costa, Petit na Luis figo
washambuliaji: Pauleta na Joao Pinto
Wachezaji wa akiba: Nuno Gomez, Paul Bento na Jorgi Andrade
Waliotoka: Rui Jorgi dk ya 69 Jorge Costa dk ya 74 na Rui Costa dk 84
Kocha Wa ureno alikua ni Antonio Oliveira

Marekani Brad Friedel golini
Mabeki: Anthony sanneh, Eddie Pope, Jeff Agoos na Frankie Hejduk
Viungo: Stewart John(Nahodha), John O’Brien, Pablo Mastroen na Darmacus Bewslay
Washambuliaji: Brien Mcboiede na Landan Donovan
Waliokua benchi : Cobi,Joe Max na Carlos
Wliingia kuchukua nafasi za Stewart dk ya 46 Landon Donovan dk ya 75 na Eddie Pope dk ya 80
kocha wao alikua Bruce Arena

Brien McBride Wa marekani alichaguliwa kuwa mchezaji bora Wa mechi hiyo.
Refa alikua Byron Moreno(Ecuador)
Refa msaidizi Bomer Fierro(Ecuador)
Na Awni Hassounah (Jordan)
Refa Wa NNE ni Saad mane (Kuwait)

Comments

0 comments:

Post a Comment