Iago
Aspas akiifungia bao la kusawazisha Hispania dakika ya 90 na ushei
katika sare ya 2-2 na Morocco kwenye mchezo wa Kundi B Kombe la Dunia
Uwanja wa Kaliningrad, Urusi. Bao lingine la Hispania limefungwa na Isco
dakika ya 19, wakati mabao ya Morocco yamefungwa na Khalid Boutaib
dakika ya 14 na Youssef En-Nesyri dakika ya 81. Hispania imemaliza
kileleni mwa Kundi B kwa pointi zake tano sawa na Ureno na zote
zinakwenda 16 Bora
Home
»
»Unlabelled
» ASPAS AIPELEKA HISPANIA 16 BORA KOMBE LA DUNIA
Tuesday, June 26, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment