Monday, June 18, 2018


Klabu ya Norwich City FC imeridhia ofa ya pauni milioni 20 kutoka kwa Leicester ili kumuachia kiungo wake mshambuliaji, James Maddison mwenye umri wa miaka 21 kujiunga na Mbweha hao wa Uingereza.

Maddison anayekipiga kwenye timu ya vijana ya Uingereza anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii tayari kujiunga na Leicester baada ya kuhuhusishwa kwa muda mrefu kuhamia Southampton.

Kinda huyo wa Norwich amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 15 kwenye michezo yake 49 aliyocheza msimu uliyopita huku klabu hiyo ikitarajia kuvuta mkwanja huo mrefu ukilinganisha na wachezaji wake wengine waliyopata kuwauza.

0 comments:

Post a Comment