Friday, June 1, 2018


Jezi mpya ambazo timu ya taifa ya Nigeria itazitumia katika mashindano ya kombe la dunia huko nchini Urusi zimenunuliwa zote kwa dakika mbili tu baada ya kutambulishwa sokoni kwa mara ya kwanza ijumaa hii asubuhi jijini London kwenye duka la kampuni ya Nike.

Kwa mujibu wa kampuni ya Nike walikuwa wameshapokea oda ya watu Milioni 3 wakitaka kununua fulana ya jezi hizo kabla ya kuachiwa ijumaa hii asubuhi.
Jezi hizo za taifa la Nigeria zinatajwa kuwa ndio jezi nzuri kuzidi jezi nyingine zitakazotumiwa na mataifa mengine kwenye kombe la dunia na ndio kwa sababu hiyo iliwalazimu kampuni ya Nike  kusogeza muda mbele wa kuziachia jezi hizo kutokana na uhitaji mkubwa.
Aidha fulana moja tu ya jezi hiyo inauzwa £64.95 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi 197,430 za kitanzania.
Kwa sasa jezi hizo hazipatikani kwenye mtandao wa kampuni ya Nike kwa sababu zimeisha kabisa.

0 comments:

Post a Comment