Friday, June 1, 2018


Na Azizi-Mtambo
Wakati klabu ya Yanga, chini ya kocha Muholanzi, Hans Van Der Pluijm, inatoa kitita cha Million 30, kumnunua beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent Chikupe(Dante), wengi mno waliona kuwa klabu hiyo ilikosea kumsajili beki Huyo.
Vicent, alikubali kusaini klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka 3 kuitumikia klabu hiyo.
Wakati anajiunga na klabu hiyo alikutana na changamoto nyingi zaidi ikiwemo kupata namba Katika kikosi hicho alikutana na baadhi ya nyota kadhaa katika eneo lake mtu kama Kelvin Yondani, Andrew Bossou, na nahodha wao Haroub Cannavaro.
Msimu wake wa Kwanza hakucheza mechi nyingi sana kwa sababu alikuta timu teyali ipo kwenye muunganiko mzuri wa safu ya ulinzi ikiongozwa na Nadir Haroub Cannavaro, akicheza sambasamba na Kelvin Yondani.
Msimu wake wa Kwanza Mwaka 2015/16, alitwaa makombe mawili yakiwemo FA cup, ligi kuu vpl, alianza kupata nafasi baada ya Cannavaro, kupata majeruhi ya mara kwa mara.
Msimu unaofuata alitengeneza safu nzuri ya ulinzi ya kati akiwa yeye na Yondani, na kusifika moja ya safu bora Kabisa katika ligi kuu.Dante anasifika zaidi kwenye kupandisha timu kuanzisha mashambulizi kukaba amekuwa nguzo nguzo nzuri ya Yanga, katika eneo hilo alishinda kombe la ligi kuu Vpl.
Vicent, Amekosa uzoefu katika mechi za kimataifa Mara nyingi akicheza na Yondani, amekuwa akitulia zaidi eneo hilo kwa sababu amepata mchezaji mwenye uzoefu na mashindano hayo ya kimataifa.
Mchezo wao wa kombe la Shirikisho Barani Afrika walipocheza dhidi ya USM Algeria, Vicent, alicheza eneo la ulinzi dhidi ya Abdallah Shaibu, walifungwa magoli 4-0 ukiangalia katika eneo hilo wachezaji wote wamekuwa hawana uzoefu wa hali ya juu? Nilimsika Vicent, alisema tumefungwa kwa sababu mie na Shaibu, hatuna uzoefu na michuano hii pia tumekutana na washambuliaji walio na ubora na wenye uzoefu kwa haraharaka alikuwa akimaanisha kumkosa nahodha wao Yondani, ilipelekea Yanga, kufanya vibaya kwenye eneo hilo.

Mchezo wa pili uliofanyika dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda, maneno ya Vicente, yalitupa majibu Tosha mchezo huo nahodha wao Yondani, alirudi na kuongoza jeshi alisimama na Vicente, na kucheza katika ubora wa Hali ya juu?mpira ulivomalizika benchi la ufundi la Rayon Sports, walimpa Sana hongera nahodha huyo kwa kuonesha ubora wa hali ya juu.
Mkataba wake umefikia tamati swali linakuja viongozi wa Yanga, watampa mkataba beki huyo ambaye amekuwa katika ubora wake.
Me binafsi uchezaji wa Vicente, namfananisha na beki wa klabu ya Liverpool, Van Djik

0 comments:

Post a Comment