Ukisema matumaini ya Waafrika kwa wawakilishi wao watano wa Kombe la Dunia huko Urusi yamekuwa finyu, hautakuwa umekosea.
Tunisia
imekuwa timu ya nne ya Afrika kupoteza mechi mechi ya kwanza na kesho
ni zamu wa Senegal. Hata hivyo, Tunisia pia imekuwa timu ya kwanza ya
Afrika kufunga bao katika Kombe la Dunia 2018.
Sasa
timu zote nne za Afrika zimecheza mechi ya kwanza na kupoteza baada ya
mechi ya jana ya Tunisia ambayo ilifungwa na England, Harry Kane
akifunga bao katika dakika ya 90.
Kabla
ya Tunisia, timu tatu za Afrika zilishacheza na kupoteza na hakuna
iliyofunga bao. Timu ya 5 ya Afrika ni Senegal, itacheza kesho dhidi ya
Poland. Kumbuka hakuna iliyoshinda wala kupata sare katika mechi zote za
kwanza.
Matumaini
ya kuwa Senegal ni timu ya mwisho ya Afrika inayocheza leo kama kweli
itaweza kuwabeba Waafrika na kuibua matumaini kama kweli kuna timu ya
Afrika inaweza kusonga mbele.
MATOKEO:
Misri 0-1 Uruguay
Morocco 0-1 Iran
Croatia 2-0 Nigeria
England 2-1 Tunisia
0 comments:
Post a Comment