Mchezaji
wa klabu ya Liverpool raia wa Uingereza, Rhian Brewster amezua gumzo
kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana kukosea neno
‘unstoppable’ kwenye ‘tattoo’ yake aliyochora kwenye mkono.
Mapema
hii leo, Brewster mwenye umri wa miaka 18 ametupia picha inayomuonyesha
akiwa kwenye uzi wa Liverpool huku mkono wake wa kushoto kukiwa na
‘tattoo’ hiyo yenye maneno yanayo someka ‘your hate makes me
unstoppable’ (Chuki zako haziwezi kunizuia).
Kwenye
tattoo hiyo iliyopo chini ya mchoro wa mpira na dunia imekosewa herufi
moja imeandikwa ‘unstopable’ ikipungua herufi ‘p’ moja badala ya neno
sahihi ‘unstoppable’.
Wachambuzi
wa mambo wanadai kuwa tattoo hiyo ni mpya kwenyemwili wa Brewster
kutokana kutokuonekana nayo wakati wa mchezo wa fainali ya michuayo ya
kombe la dunia kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 wakati timu
ya taifa ya Uingereza ilipotwaa taji hilo nchini India mwezi Oktoba
mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment