Tuesday, October 12, 2021



BONDIA Abdallah Shaaban Pazi ‘Dullah Mbabe’ jana aliwasononesha Watanzania baada ya kuchapwa kwa pointi na Tshimanga Katompa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika pambano la raundi 10 ukumbi wa PTA, Temeke Jijini Dar es Salaam.
Dullah ambaye Agosti 20 alishindwa pia kwa pointi na Mtanzania mwenzake, Twaha Kassim ‘Kiduku’ – hakuwa katika ubora wake kabisa jana baada ya kuangushwa mara tatu ndani ya raundi ya saba, kabla ya kumalizia raundi tatu za mwisho na kuepuka kipigo cha Knockout. 

0 comments:

Post a Comment