Thursday, October 7, 2021

 

 TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la COSAFA baada ya ushindi wa penalti 3-0 kufuatia sare ya 1-1 na Zambia mchana wa leo Uwanja wa Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Shujaa wa Twiga Stars leo alikuwa ni kipa, Janet Simba aliyeokoa mikwaju miwili ya penalti ya Zambia. 
Finali ni Jumamosi na Twiga Stars itamenyana na Malawi iliyoichapa Afrika Kusini 3-2 jioni ya leo katika Nusu Fainali nyingine hapo hapo Port Elizabeth. Zambia na Afrika Kusini watawania nafasi ya tatu mapema Jumamosi.


0 comments:

Post a Comment