Friday, August 17, 2018



Club ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta leo iliingia uwanjani kucheza game yake ya marudiano ya kuwania kucheza hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya Lech Poznan ya Poland.
KRC Genk ikiwa ugenini nchini Poland katika game ya marudiano baada ya game ya kwanza nyumbani Luminus Arena kupata ushindi wa magoli 2-0, leo tena wamepata ushindi mwingine wa magoli 2-1.

Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 19 na Trossard kwa mkwaju wa penati dakika ya 45 wakati goli pekee la Lech Poznan lilifungwa na Cywka dakika ya 50. Hii ni game ya pili mfululizo Mbwana Samatta anaifungia goli KRC Genk.

0 comments:

Post a Comment