Mshambuliaji wa
Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 21, amekuwa akijivinjari na
wachezaji wa Arsenal wakati wa likizo , na kuongeza uvumi kwamba huenda
akajiunga na the Gunners. (Goal.com)
Ajenti wa kipa wa Chelsea
Thibaut Courtois ameitaka Chelsea kumwachilia mchezaji huyo wa Ubelgiji
mwenye umri wa miaka 26, kuhamia katika klabu ya Real Madrid. (Sun)Liverpool ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27, kutoka Arsenal. (Express)
Mshambuliaji wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial, 22,huenda akasalia katika klabu hiyo ya Old Trafford kwa kuwa mkufunzi Jose Mourinho hataki kumuuza hadi atakapopata mchezaji mbadala kuchukua mahala pake. . (Mirror)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana mpango wa kumnunua beki wa Croatia na Besikitas Domagoj ,29,Vida kwa dau la £25m. (Sun)
Winga wa Monaco na Algeria Rachid Ghezzal, 26, anatarajiwa kujiunga na Leicester kwa dau la £12.5m. (L'Equipe - in French)
West Ham wameimarisha hamu yao ya kutaka kumnunua winga wa Brazil Bernard, 25, ambaye bado hajapata klabu baada ya kutoka Shakhtar Donetsk mwisho wa msimu uliopita (Guardian)
Ombi la Burnley la dau la £15m kwa beki wa Uingereza Ben Gibson, 25, limekubaliwa na klabu ya Middlesbrough. (Mail)
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 03.08.2018:
Image caption
Real Madrid wameweka gharama ya £670m kwa atakayetaka kumnunua Mcroasia-Luka Modric
Real Madrid
wameweka tangazo la kiwango cha bei ya £670m kwa mchezaji wa miaka 32
wa kiungo cha kati wa timu ya Croatia -Luka Modric, aliyetajwa kama
mchezaji bora wa Kombe la Dunia la 2018, kuizuwia Inter Milan kujaribu
kumchukua. (Mirror)
Manchester
United imeafiki masharti binafsi ya mlinzi wa Barcelona Yerry Mina,
mwenye umri wa miaka 23, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia
akisubiri klabu ziukubali mkataba . (Metro, via Mundo Deportivo)Winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 25, amewaambia wachezaji katika timu yake kwamba yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anaweza kuwasilisha maombi ya kuhamia Chelsea. (Mirror)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amejipanga kwa mazungumzo na mlinda lango Thibaut Courtois, huku Real Madrid wakiwa tayari kusaini mkataba na Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 26 . (Diario AS, via Star)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumtoa mshambuliaji wake kutoka Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, kwa Bayern Munich kama sehemu ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29. (Mirror)
Bournemouth watatakiwa kutoa £30m ili kuwashawishi Levante kumtoa mchezaji wao safu ya kati wa Colombia Jefferson Lerma, mwenye umri wa miaka 23, baada ya the Cherries kuwa kukataliwa pendekezo lao. (Sun)
Burnley walikataliwa pendekezo lao la £11m Middlesbrough la kumnunua mchezaji wa safu ya ulinzi Muingereza Ben Gibson, huku Everton pia wakionyesha azma ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Northern Echo)

Mchezaji wa Anderlecht anayechezea safu ya kati ya Ubelgiji Leander Dendoncker, mwenye umri wa miaka 23, amekataa kuhamia katika Ligi ya Primia , kwa kukataa Crystal Palace na Wolves kwa pamoja . (Sun)
Hata hivyo , Wolves wako tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ili kumuweka kibindoni mchezaji wa Middlesbrough na Winga wa Uhispania Adama Traore, mwenyeumri wa miaka 22. (Telegraph)


0 comments:
Post a Comment