Unai Emery ajitetea baada ya Vijana wake kupokea kipigo kutoka kwa Manchester City
Kocha mpya wa klabu ya Arsenal aliyejiunga nao msimu huu akitokea PSG ya Ufaransa Unai Emery amejitete kwa staili ya aina yake baada ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa vijana wa Pep Guardiola Manchester City.
Arsenal wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi kuu nchini Uingereza ambao uliochezewa katika viunga vya Emirates Stadium Jijini London wakiwa nyumbani,Man City walianza kufungua ukurasa wa magoli mnamo dakika ya 14 baada ya Sterling kuwachambua mabeki wa Arsenal na kuumalizia mpira huo huku mlinda mlango wa Arsenal Cech akiusindikiza mpira huo kwa macho,huku goli la pili likipatikana dakika ya 64 baada ya Bernando Silva kuupeleka mpira huo kimiani baada ya kupokea mpira kutoka kwa Benjamin Mendy na kuifanya Man City kujihakikishia alama tatu muhimu Ugenini.
The Gunners wameanza mchezo wao wa kwanza wakiwa na kocha mpya baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 20 wakiwa chini ya Mfaransa Arsene Wenger,ambaye alitangaza kustaafu kuinoa klabu hiyo mapema katika dirisha kubwa la usajili.
Emery ameongea katika Press baada ya mchezo wao na kusema “Nadhani Man City walistahili matokeo haya, Ingawa tulijitahidi kurekebisha makosa yetu wakati wa dakika 90,lakini nadhani tunahitaji muda zaidi,hadi kufikia wiki ijayo katika mechi inayofuata nahisi tutakuwa sawa, “Emery alisema katika mkutano huo na Wanahabari.” Na katika nusu ya pili ya mchezo tulikuwa na nafasi nzuri ya kufanya matokeo yawe mazuri zaidi lakini ilishindikana”
“Huu ndio mchezo wangu wa kwanza katika timu hii nadhani hata mbinu bado mpya ukilinganisha na Man City ambao wamekuwa katika mbinu zao ndani ya miaka mitatu wakiwa na Guardiola na pia wameijenga timu yao kwa muda na wakiwa na wachezaji bora zaidi wakiwa na utulivu zaidi wakicheza wanavyotaka”
katika mchezo ujao Arsenal watakuwa Ugenini mitaa hiyo hiyo ya London kukutana na vijana wa Sarri Chelsea katika Dimba Stamford Bridge.
0 comments:
Post a Comment