Thursday, August 16, 2018



Leo nilikuwa napoga stori na marafiki zangu. Nikawaambia Mafanikio aliyopata Antoine Griezmann msimu huu, kama angeyapata Messi au Ronaldo mmoja wao yaani (Messi au Ronaldo angepelekeea tu tuzo zake nyumbani). Wala pasi gekuwepo naa haja ya kupiga kura za mchezaji bora. Nsdhani kwa suala la mafanikio Antoine Griezmann anastahiki pongeza kwa mafanikio yake hasa ya kitimu.
Bila shaka wafaransa huu ni mwaka wao. Yaani katika ile Orodha ya makombe makubwa au maarufu duniani kuna mfarannsa kaweka mkono wake pia.
Uefa imebebwa na Madrid
Alikuwa Varane ambaye ni beki kisiki wa klabu hiyo. Kombe hilo hajalibeba kwa wasiwasi au akiwa benchi. Hapana. Alishirikia kwa asilimia 99. Ni mmoja wa mashuja waliofanikisha kombe la tatu mfululizo.

Uefa Super Cup na Europa league:
Arsenal walitwangwa na Atletico tena Griezmann akiwahukumu kwa mabao ya kizembe. Kisha fainali wakakutana na Marseille ambapo kufila kwao fainali ya Europa league pia ni ishara tosha kuwa Ufaransa mwaka huu kweli walipania kila idara. Tumeona jana Griezmann, Fernandez pamoja na Lemar wakiondoka na ndoo yao ya Uefa Super Cup.
Kwa upande wa ligi mbalimbali
EPL
Benjamini Mendy amefanikiwa kutwaa kombe hilo. Americ Laporte pia ni mfaransa licha ya kwamba kwa bahati mbaya hakuweza kujumuishwa kikosi cha tiMu yake ya taifa.
FA Cup na Carling Cup pamoja na ngao ya hisani:
FA imebebwa na Chelsea waliokuwa wakiongozwa na Oliver Giroud pamoja na Ngolo Kante. City walibeba Carling Cup wakiwa na pia Benjamini Mendy

La liga, Copa de la rey, na Spanish Supa Cup:
Barcelona wamebeba Laliga na makombe hayo mengine yote. wakiwana Ousumane Dembele pamoja na beki kisiki Samuel Umtiti. Lucas Digne pia ni mfaransa lakini kwa bahati mbaya timu ya taifa hakuitwa.
Bundasliga na DFB pokal
Bayern Munich wamefanikiwa kutwaa makombe hayo huku wakiwa na kiungo mfaransa Florentino Tolliso. Tolliso pia amekuwa na kiwango bora msimu kiasi cha kuitwa timu ya taifa.
Serie A na Coppa Italia
Blaise Matuidi alijiunga na wababe wa Turin na mwaka huu amefanikiwa kutwaa vikombe hivyo akitokea klabu ya Paris Saint German. Matuidi pia alikuwa miongoni mwa mashujaa wa Ze blues waliotwaa kombe la dunia.
Ligue 1: , Coupe de France: na
Coupe de la Ligue:
PSG imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ufaransa na mapema hivi majuzi pia walitwanga Monaco mabao 4. Neymar alikuwa miongoni mwa nyota waliofunga huku akifikisha mabo 21 kwenye michezo 20 katika uwanja wao wa nyumbani. PSG imesheheni nyota mbalimbali wa Ufaransa kama nyota wao Kylian Mbappe, Kurzawa na wengineo.

Kwa haraka haraka wafaransa wamefanya vizuri sana lica ya kuwa pia bahati zilikuwa upande wao.
Tuzo binafsi
Griezmann
Mchezaji bora wa Ulaya
Kkatu cha Silva Kombe la dunia
Kante
Mchezaji bora wa Chelsea
Mbappe
Mchezaji bora chipukizi kombe la dunia.
UNFP Ligue 1 mchezaji bora chipukizi: 2016–17, 2017–18
UNFP Ligue 1: Kikosi bora cha msimu 2017–18
UNFP Mchezaji bora wa mwezi: March 2018.
Varane
ametajwa kwemye orodha ya mabeki bora wa UCL

Kiujumla hamna kombe waliloliacha. Hata yale makombe ya mbuzi walibeba

0 comments:

Post a Comment