Mazungumzo
ya mkataba mpya kati ya winga wa Manchester City Raheem Sterling na
klabu yake yamegonga mwamba Sterling, 23, huku mkataba wa raia huyo wa
England ukielekea ukingoni. (Guardian)
Crystal
Palace imeulalamikia Uongozi wa Ligi Kuu Uingereza kwa kushindwa
kumlinda staa wao Wilfred Zaha, 25, ambaye pia ni raia wa Ivory Coast
anaokuwa uwanjani akicheza. (Telegraph)
Mkurungezi
wa michezo wa Roma Monchi amesema walilazimika kumuuza mshambuliaji wa
Misri Mohamed Salah, 26, kwenda Liverpool kwa sababu ya Sheria ya
Uchezaji Haki Kifedha michezoni. (El Mundo)
Beki
wa zamani wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Steven Caulker,
26, anaweza akajiunga na klabu kutoka Ukraine, Arsenal Kiev baada ya
kuahidiwa dili na kocha wa klabu hiyo Fabrizio Ravanelli ambaye pia
amewahi kuwa mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough. (Mirror)
Beki
wa zamani wa Chelsea, John Terry, 37, hajaamua bado kama ataendelea
kucheza baada ya kukataa kujiunga na klabu ya Urusi Spartak Moscow.
Aston Villa imeonyesha nia ya kumsainisha tena beki huyo. (Birmingham
Mail)
Rais
wa FiFa Gianni Infantino amesema ana mashaka kuhusu kuufanya mchezo
kati ya Barcelona dhidi ya Girona wa La Liga kuhamishiwa katika uwanja
wa Hard Rock nchini Marekani. (ESPN)
Crystal
Palace, Brighton and Watford zinamtolea macho kinda Adam Lovatt, 18,
anayecheza katika klabu ya Bostik kwenye mashindano ya kanda ya kusini
mashariki nchini Uingereza. (Team Talk)
Klabu
ya Crystal Palace imemsajili Barry Simmonds kutoka Fulham kuungana na
kocha wake wa zamani Roy Hodgson kama mapendekezo yake. Barry alikuwa
mzuri sana katika kuwatafuta wachezaji nyota na ndiye aliyechangia
kupatikana kwa Mousa Dembele, Chris Smalling na Zoltan Gera. (Mail)
Kutoka BBC
0 comments:
Post a Comment