Southgate mwenye umri wa miaka 48, anatarajia kusaini karatasi za mkataba kabla vijana wapya hawajajiunga na kikosi cha taifa huko St George Park siku ya Jumapili jioni.
Dili hilo linajumuisha kuongezewa kima cha mshahara kwa asilimia 50 hii inatokana na kuiwezesha Uingereza kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2018.
Mkurugenzi wa chama cha soka England (FA), Martin Glenn amesema kuwa hawakuweza kukamilisha hiyo biashara na uongozi wa Southgate nchini Urusi na lengo kuu ni kuwa kwenye nafasi ya nne duniani kwenye viwango vya FIFA.
Southgate anatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Alhamisi hii huko St George’s Park ili kutangaza kikosi kitakacho jiandaa na Nations League mechi dhidi ya Croatia na Hispania.
0 comments:
Post a Comment