
Maneno ya Mourinho yanakuja wakati akitarajia kushuka uwanjani hapo kesho siku ya Jumanne kukabiliana na Valencia mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya.
Mreno huyo amekuwa kwenye kipindi kigumu na kukosa kujiamini tangu United kushindwa kufanya vizuri mwanzoni mwa msimu huu na hata kushindwa kuonyesha makali mbele ya Derby County na West Ham huku akihusishwa kutimuliwa kama meneja wa mashetani hao wekundu.

Mourinho amesisitiza kuwa wapo baadhi ya wachezaji anao elewana nao ma kumuamini huku wakimjali zaidi ya hao wengine.
Alipoulizwa na waandishi wa habari mchana wa leo juu na fasi yake kama ameshaongea na makamu mwenyekiti wa United, Ed Woodward amesema kuwa hayo ni mambo binafsi.
0 comments:
Post a Comment