Baada ya hilo kutokea kumekuwa na sintofahamu ikielezwa kuwa kuna mvutano kali sana kwenye klabu hiyo ikisemekana kuna mgawanyo wa wachezaji wengine wakiwa upande wa Pogba huku wengine wakiwa upande wa Mourinho.
Mgongano huo ukiendelea kuna tetesi za kuwa huenda aliyekuwa kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane kudaiwa kuja kurithi mikoba ya Mreno huyo.
Baada ya timu hiyo kupata matokea mabaya dhidi ya West Ham siku ya jumamosi kumekuwa na maneno pia kuna mgogoro mkubwa sana katika ya wachezaji viongozi na kocha huyo wengi wakisema kocha huyo aondokelewe kwenye timu hiyo,huku siku ya jumamosi kulikuwa na mabango mengi sana yakimtaka kocha huyo aondoke kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.
Kupitia ESPN mchezaji wa timu hiyo pia Muingereza Luke Shaw ameibuka na kumtetea kocha huyo akida Mourinho hana tatizo bali tatizo lipo kwa wachezaji.
“Tunapaswa kujiangalia sisi wenyewe kama wachezaji, “alisema Shaw.” Sisi ndio ambao tunaingia uwanjani, Kocha haingii uwanjani Yeye yuko nje ya uwanja ili kuiweka timu sawa akiwa nje bali ndani inakuwa wajibu wetu”

“Kwa mfano Ukiiangalia timu yetu dhidi ya West Ham na tulikuwa na timu nzuri na yenye nguvu sana na Hatukuna na sababu kabisa”.
“”Sio vizuri kabisa Ni vigumu kuchukua kuamini kwa timu kama Manchester na vipaji vyote iliyonavyo lakini sisitunawashukuru sana mashabiki.”
” kutoka dakika ya kwanza ukiwa unaagalia mpira huoni kabisa nafasi na kuona kama timu inashinda hii sio nzuri kabisa kwetu “Michezo kama hii tunapaswa kutawala, na tunapaswa kutengeneza nafasi nyingi pia kuonyesha watu kwa nini sisi tunastahili kuchezea na Man United na haikutokea tu.”
0 comments:
Post a Comment