Friday, July 26, 2019


BARCELONA wameamua kutoa listi ya wachezaji sita kwa PSG ili ikubai kukamilisha dili la kumpata mchezaji wao wa zamani, Neymar Jr.

Inaelezwa kuwa Barcelona wameamua kufanya hivyo ili kuwashawishi PSG wakubali ofa yao ya pauni milioni 90 sawa na bilioni 257.

Wachezaji ambao wamewekwa kwenye listi ni pamoja na Philippe Coutinho, Ousmane Dembele, Ivan Rakitic, Nelson Semedo na Malcom, mchezaji wa sita hakujulikana mara moja.

Neymar ameweka wazi kuwa anataka kusepa na PSG inasemekana imekubaliana na maombi ya staa huyo ila haitaki ofa ndogo wao wanataka dau lao la pauni milioni 198 (bilioni 567) ambazo walizitoa kwa Barcelona mwaka 2017.

0 comments:

Post a Comment