Monday, July 29, 2019


HAJI Manara ni kama amewatupia dongo wapinzani wake Yanga kiaina kutokana na kauli yake kwamba wengi wamewaiga siku ya Simba day na wameiga kwa mpango mdogo.

Manara amesema kuwa wengi wanaiga mpango wao wa kuwa na siku maalumu ya kuwatambulisa wachezaji na bado hawajafikia hatua ya ubora ambao Simba wapo kwa sasa.

"Wengi tunaona wanaiga, kuna wale ambao wapo Kenya, Uganda na sehemu nyingine tunaskia wana maandamano kabisa hivyo hayo ni maono madogo.

"Sisi tunakuja kikazi na kauli mbiu yetu ya Simba day msimu huu ni SpotiPesa Simba wiki, iga ufe, huwezi kuiga tu kitu bila ya kuwa na mpango mzuri, masuala ya maandamanomaandamano kwetu tulishamaliza kitambo tunaangalia mambo mengine, hii mambo sijui ya kusema namna gani vipi kwetu hakuna.

"Sisi ni hatua nyingine kabisa kwa sasa kuna watu wa Kenya, Uganda nao wanaiga hivyo tunafanya kazi kubwa, tumejipanga kisawasawa," amesema.

0 comments:

Post a Comment