Monday, July 29, 2019



TOWNSHIP ROLLERS

Mbelgiji Mbelgiji Patrick Aussems ambaye ni Kocha wa Mabingwa wa Tanzania, Simba amewaonya Yanga kuhusiana na wapinzani wao kutoka Botswana.


Aussems amewaambia wapinzani wao Township Rollers ambao watacheza nao katika Ligi ya Mabingwa Afrika wapo vizuri na wasiwadharau.


Aussems amesema hayo ikiwa ni baada ya kucheza na Rollers katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu ambao ulipigwa juzi Jumamosi katika Jiji la Rustenburg, Afrika Kusini na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.


Yanga wamepangwa kucheza na Rollers katika Ligi ya Mabingwa ambapo watakutana katika mechi ya kwanza kati ya Agosti 9-11 na kisha baadaye kwenda kurudiana nchini Botswana.


Aussems raia wa Ubelgiji amesema kwamba Rollers wamekuwa kipimo tosha kwa klabu yake tangu walipocheza mechi za kirafiki Afrika Kusini na amewaona wapo tayari kwa ajili ya mechi za kimataifa.



“Nimeridhika tumecheza na timu ambayo ipo tayari kwa Ligi ya Mabingwa na imekuwa nzuri kwetu kwa kutuonyesha wapi ambapo tunatakiwa kufanyia kazi.

0 comments:

Post a Comment