PATRICK
Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ana kazi ngumu ya kufanya kwa
sasa baada ya nyota wake kujiunga na timu ya Taifa.
Kocha
huyo amedai kuwa wachezaji hao wataharibu mipango yake kwenye mechi
yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na muda ambao
watakaokaa ndani ya kambi ya Stars.
Aussems
amesema kuwa wachezaji hao watarudi siku chache kabla ya mechi yao hiyo
ya kimataifa ambapo wamepangwa kucheza na UD do Songo ya Msumbiji kati
ya Agosti 9 hadi 11.
“Wachezaji
hao ambao wameenda Stars, kwa namna fulani wametibua mipango yangu kwa
sababu watarudi siku mbili kabla ya sisi kucheza na UD Songo.
“Wakija ni lazima wapewe mafunzo maalum ili wawe sawa na wenzao, kitu ambacho unaona kinatibua mbinu zangu,” amesema Aussems.
Aussems
ataiongoza Simba kwenye michuano ya kimataifa kwa mara ya pili
mfululizo ambapo kwa msimu huu watacheza na mabingwa wa Msumbiji UD do
Songo.
Mechi
ya kwanza watacheza nchini Msumbiji Agosti 9-11 na watarudiana Dar es
Salaam Agosti 23-25 na baadhi ya nyota ambao wapo timu ya Taifa ni
nahodha John Bocco na Ibrahim Ajib.
0 comments:
Post a Comment