Thursday, July 25, 2019


Paris St-Germain wameishinda Juventus katika kinyang’anyiro cha kumsaini mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, na wanaamini watafikia mkataba wa pauni milioni 20 kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England . (Sun)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, yuko tayari kuongeza bei ya Toby Alderweireld,30 hadi pauni milioni 40 ikiwa mkataba unaodhibiti uhamisho wa mchezaji huyo raia wa Ubelgiji utakufikia kikomo chakaIjumaa hii. (Telegraph)
Naibu mwenyekiti mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yuko mbioni kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wapya, zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kukamilia. (ESPN)
Woodward ana matumaini ya kukamilisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City, Harry Maguire, 26, na mchezaji wa safu ya kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (London Evening Standard)
Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMlinzi wa England na Leicester City, Harry Maguire
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana wiki mbili kuamua ikiwa atamuachilia winga wa England wa chini ya miaka-21 Reiss Nelson, 19, kujiunga na Hertha Berlin kwa mkopo msimu ujao. (Sun)
Mkufunzi wa Celtic Neil Lennon, anatarakiwa kufanya mazungumzo na beki wa Scotland Kieran Tierney, 22, baada ya ofa ya tatu ya Arsenal ya kumnunua mchezaji huyo kukataliwa. (Daily Record)
Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis Muargentina Giovani lo Celso, 23, kwa kima cha pauni milioni 45. (Sun)
Giovani Lo Celso in action against Real MadridHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLo Celso scored 16 goals for Real Betis last season
Mchezaji wa safu ya kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24, amesema kuwa ataendelea kucheza katikaligi kuu ya Ureno licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Mirror)
Sporting na Manchester United bado hawajakubaliana kuhusu bei ya Fernandes. Klabu hiyo ya ligi kuu ya England imesalia na £7m kufikia bei ya kununua nyota huyo wa Ureno anayekadiriwa kuwa £62m. (Star)
Bruno FernandesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBruno Fernandes
Liverpool haitamruhusu kiungo wa kati wa England mwenye umri wa chini ya miaka -21 Ovie Ejaria kuondoka klabu hiyo kwa mkopo msimu huu – lakini wako tayari kumuuza mchezaji huyo. (Liverpool Echo)
Mlinzi wa Manchester City Tosin Adarabioyo, 21, ambaye msimu uliopita alikuwa West Brom kwa mkopo, anajiandaa kujiunga na Blackburn. (Manchester Evening News)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado anapania kumnunua mchezaji mwingine mmoja msimu huu. (Liverpool Echo)
Jurgen Klopp celebrates

0 comments:

Post a Comment