MENEJA wa Sporting CP, Marcel Keizer amesema kuwa mchezaji wake Bruno Fernandez anaweza kujiunga na Manchester United.
Kiungo huyo alikuwa kwenye rada za United kabla ya Keizer kusema kuwa hawezi kumuachia kwa kuwa yupo kwenye mipango yake.
"Kila mmoja angependa abakie ndani ya timu kutokana na uwezo wake na msaada anaoutoa ndani ya timu ila kwa sasa hatujui kitakachotokea mbele ni jambo la kusibiri na kuona," amesema.
Dau la nyota huyo linatajwa kuwa pauni milioni 62 hivyo United wakiweka mezani wanampata kiungo huyo, ambaye amefunga mabao 20 katika mechi 30 za mashindano yote na kutoa assit 13.
0 comments:
Post a Comment