Friday, July 26, 2019


Dar es Salaam.Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta amevunja ukimya kwa kusema Genk siyo gerezani, hii klabu ni familia yangu. Kwa pamoja tumefanikiwa kutwaa ubingwa na tutacheza Ligi ya Mabingwa. Kwa hiyo kwanini niondoke.

Tangu mwisho wa msimu huu Samatta amekuwa akihusishwa na kutakiwa na timu mbalimbali za England, Leicester City, Watford, Aston Villa, Cardiff City, pia SS Lazio ya Italia na sasa Galatasaray ya Uturuki.

Akizungumza na wanahabari nchini Ubelgiji, Samatta alisema kazi yangu ni kucheza mpira, sitaki kuweka akili kuzungumzia kuhusu tetesi zinazoendelea juu yangu kwa sasa kama kuna timu inayonitaka waje mezani tuzungumze.

“Meneja wangu anajua hilo. Nataka kuwa peke yangu kwa siku mbili kabla ya ligi kuanza kufanya uamuzi. Kama itakuja timu inayonitaka kweli nipo tayari kuwasikiliza."

Samatta alisema kuna wakati sifikiri kuondoka Genk. "Genk siyo gerezani, hii klabu ni familia yangu. Kwa pamoja tumefanikiwa kutwaa ubingwa na tutacheza Ligi ya Mabingwa. Kwa hiyo kwanini niondoke? Wakati hapa ni furaha,” lilimnukuu gazeti la Fanatic.

0 comments:

Post a Comment