Caster Semenya
anasema hatotetea taji lake la ubingwa wa mbio mita 800 duniani mwezi
Septemba kufuatia uamuzi dhidi ya kesi aliyowasilisha mahakamani
kupinga, kuidhinisha viwango vya homoni ya testosterone miongoni mwa
wanariadha wanawake.
Lakini mwanariadha huyo wa Afrika kusini
amesema "ataendelea kupambana kutetea haki za binaadamu" licha ya
"kusikitishwa kwake". Semenya amewahi mara mbili kukata rufaa dhidi ya sheria za IAAF zinazomzuia kukimbia pasi kutumia dawa.
Lakini uamuzi unaomruhusu kukimbia sasa umebatilishwa.
- Castor Semenya: Kwanini kesi yake ni muhimu
- Caster Semenya kuwa mtetezi wa jinsia
- IAAF limekana Semenya atambulike kama mwanamume
Semenya alikuwa anaweza kukimbia wakati kukisubiriwa uamuzi wa mahakama ya Uswizi, na akiwa awali alishindwa katika rufaa aliyowasilisha katika mahakama inayoshughulikia mizozo katika michezo (Cas) mnamo Mei.
Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa Twitter, Semenya ameandika muda mfupi uliopita, "Nafsi inayojitahidi haiwezi kuzuilika" baada ya kushindwa katika kesi hiyo.
Uamuzi huu wa sasa wa mahakama ya juu zaidi ya Uswizi una maana kuwa hatoruhusiwa kushindana katika mashindano ya ubingwa duniani huko Doha.
"Nimesikitishwa sana kuzuia kulitetea taji langu nililioshinda kwa ugumu," Semenya, mwenye umri wa miaka 28, amesema.
"Lakini hili halitonizuia kuendelea kupambana kutetea haki za binaadamu kwa wanariadha wote wanawake waliohusika."
IAAF limesema linataka sheria hizo zilizosimamishwa ziidhinishwe kuepuka "mchanganyiko mkubwa" miongoni mwa wanariadha na waandalizi wa mashindano na "kulinda hadhi ya mchezo".
Limnepinga tuhuma katika barua kwamba sheria zake "zinashinikiza ukosefu wa usawa wa kijinsia", na kwa kujibu limeeleza kuwa sheria hiyo iliidhinishwa "mahsusi kwasababu IAAF inawajibika kulinda haki na fursa za wanariadha wanawake".
- Uingereza yalaumiwa kutumia ''ukatili'' kuiteka meli ya Iran
- Ni kweli 'Yesu Kristo' amefika Kenya?
- Sudan yafunga shule zote baada ya mauaji ya wanafunzi
Dorothee Schramm, wakili aliyongoza rufaa ya Semenya aliongeza: "Uamuzi wa jaji hauna athari kwa rufaa yenyewe. Tutaendelea kuifukuzia rufaa ya Caster na kuzipigania haki zake msingi za binaadamu. Mashindano huamuliwa mwisho."
0 comments:
Post a Comment