Thursday, August 15, 2019

Caster Semenya
Mshindi mara mbili wa michuano ya Olimpiki Caster Semenya amesema ''hajawahi kuhisi kuungwa mkono'' na wanawake wengine kwenye michezo.
Mshindi mara tatu wa mbio za mita 800 hatatetea taji lake mjini Doha mwezi Septemba baada ya kugonga mwamba mahakamani kuhusu kutumia dawa za kupunguza homoni za testosterone kwa wakimbiaji wa kike.
''Wananilenga kwasababu hawaniwezi,'' alisema mwanadada huyo mwenye miaka 28.
''Tangu nilipokuwa mwanamichezo, sikuwahi kwa kweli kujihisi kuungwa mkono, sikuwahi kuhisi kutambuliwa na wanawake.''
Akizungumza katika mkutano wa wanawake mjini Johannesburg, Semenya aliongeza: ''Ninafikiri
Semenya amepinga sheria mpya za mashirikisho ya mchezo wa riadha kuwa yeye na wengine kama yeye wenye kiwango kikubwa cha homoni kutumia dawa za kupunguza ili kuweza kushindana kuanzia mbio za mita 400 mpaka maili moja, au kubadili mbio watakazoshiriki.
Semenya kukosa mashindano ya ubingwa duniani
Castor Semenya: Kwanini kesi yake ni muhimu
Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m London
Semenya alikata rufaa mara mbili dhidi ya sheria zashirikisho la mchezo wa riadha IAAF zinazomzuia kukimbia bila kutumia dawa.
Kuhusu kile kinachoelezwa kutokuungwa mkono na wakimbiaji wenzie wa kike, Semenya ameongeza: ''Mimi ninafanya vizuri sana.Ukifanya vizuri duniani watu husumbuka na kutokana na unachokifanya''.
''Labda mimi ni tatizo kwasababu nina mafanikio makubwa kupitiliza hivyo , hivyo watu wanakuwa kama wanataka kukushughulikia.''
''Yeyote atakayenizuia kukimbia anapaswa kuniondoa kwenye mstari wa kukimbia. Sina cha zaidi cha kusema kuhusu suala hili. Ninachoweza kusema ni kwamba nipo kwenye kiwango cha juu.''

0 comments:

Post a Comment