Friday, August 16, 2019



Kikosi cha Polisi Tanzania kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Ushirika huko Moshi.

Yanga imepoteza mchezo huo ukiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers huko Botswana Agosti 23, 2019.

Mabao ya Polisi yamewekwa kimiani na Marcel Kaheza aliyecheka na nyavu dakika ya sita ya mchezo kwa njia ya penati.

Bao hilo lilidumu kwa dakika 45 ambazo zilimalizika kwa Polisi kuwa mbele kwa 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi tena ambapo Polisi walizidi kulisakama lango la Yanga na katika dakika ya 74, Ditram Nchimbi aliandika bao la pili.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Polisi ambao wamepanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao walikuwa na mabao hayo mawili na Yanga wakiwa na sifuri.

0 comments:

Post a Comment