PAULO
Dybala nyota wa Juventus na timu ya Taifa ya Argentina bado hajajua
afanye maamuzi gani kwa sasa kama ni kutimka ndani ya kikosi hicho na
kutafuta changamoto mpya ndani ya Manchester United.
Uongozi wa Juventus umesema kuwa ni wakati mzuri kwa nyota huyo kufanya maamuzi sahihi ili kuzuia maneno mengi ambayo yanasemwa juu yake kwa sasa.
Dybala amesema:-"Kuna ofa nyingi mkononi kwa sasa ambazo ninazitazama ila bado sijaona ipi ni bora kwangu kwa sasa, hivyo bado nasubiri wakati ukifika nitachukua maamuzi.
Nyota huyo ambaye amejiunga na Juventus msimu wa 2015/16 akitokea klabu ya Palermo ambapo alipachika jumla ya mabao 19 na assisti 8.
Msimu uliopita akiwa ndani ya Juventus alipachika mabao matano na assisti nne huku sababu za kushuka kiwango ikidaiwa kuwa ni utawala mpya wa Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na Juve akitokea Real Madrid.

0 comments:
Post a Comment