Saturday, August 24, 2019


KOCHA Mrundi, Etienne Ndayiragijje ametaja kikosi cha Tanzania kitakachomenyana na Burundi katika hatua ya awali kuwania kupangwawa kwenye makundi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Taifa Stars watakuwa wageni wa Int’hamba Murugamba Uwanja wa Taifa mjini Bujumbura Septemba 2 kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 8 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
Na leo Ndayiragijje ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30, akimrejesha kipa Beno Kakolanya wa Simba pamoja na kumjumisha mchezaji huru, chipukizi Kelvin John ‘Mbappe’ aliyeng’ara kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ya kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) mapema mwaka huu mjini Dar es Salaam.

Beno Kakolanya amerejeshwa kikosini Taifa Stars baada ya mwanzo mzuri klabu mpya, Simba SC

Baada ya kuachwa Yanga, Kakolanya ameingia na mguu mzuri Simba akianza moja kwa moja kudaka kutokana na kipa namba moja wa klabu hiyo, Aishi Manula kuwa majeruhi.
Na kwa sababu Aishi pia ndiye kipa namba moja wa Tanzania hakuna ajabu Kakolanya amerejeshwa Taifa Stars pia. 
Walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni makipa; Metacha Mnata (Yanga SC), Beno Kakolanya (Simba SC) na Juma Kaseja (KMC).
Mabeki; Boniphace Maganga (KMC), Shomary Kapombe (Simba SC), Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Gardiel Michael (Simba SC), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Iddi Moby (Polisi Tanzania), Erasto Nyoni Simba SC na Abdi Banda (Highlands, Afrika Kusini).
Viungo ni; Jonas Mkude (Simba SC), Baraka Majogoro (Polisi Tanzania), Himid Mao (ENPPI, Misri), Ally Ng’anzi (Mennesota, Marekani), Abubakar Salum ‘Sure Boy’ (Azam FC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadida), Eliuter Mpepo (Buildcon, Zambia), Hassan Dilunga (Simba SC), Mohammed Issa ‘Banka’ (Yanga SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC) na Farid Mussa (Tenerife, Hispania).
Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Abdilahie Yussuf (Blackpool, England), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Kelvin John (Huru), Ayoub Lyanga (Coastal Union) na Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC).
Mechi nyingine za awali za mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu Kombe la Dunia  Qatar 2022 ni Ethiopia na Lesotho, Somalia na Zimbabwe, Eritrea na Namibia, Djibouti na Eswatini, Botswana na Malawi, Gambia na Angola na Liberia dhidi ya Sierra Leone.
Nao Mauritius watamenyana na Msumbiji, Sao Tome na Principe dhidi ya Guinea-Bissau, Sudan Kusini na Equatorial Guinea, Comoro na Togo, Chad na Sudan na Shelisheli dhidi ya Rwanda.
Washindi 14 wa jumla wataungana na timu nyingine 26 za viwango vya juu barani, wakiwemo majirani Kenya na Uganda kugawanywa kwenye makundi 10 ya timu tano kila moja kuanza rasmi kuwania tiketi ya Qatar 2022.
Washindi wa makundi yote wataingia hatua ya tatu na ya mwisho ya mwisho ya mbio hizo za Qatar.
Loading...

0 comments:

Post a Comment