Kocha wa timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, Sebastien Migne amefukuzwa kazi ikiwa ni miezi 14 tu baada ya raia huyo wa Ufaransa kuanza mkataba wake wa miaka tatu.
Migne ambaye pia aliwahi kuhudumu kama kocha wa timu ya kitaifa ya Congo Brazzaville aliachishwa kazi jana, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Kenya (FKF).
“FKF ingependa kumshukuru Migne kwa huduma zake ambazo ziliwezesha timu ya kitaifa kufuzu mashindano ya AFCON mwaka wa 2019 mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 15,” FKF ilisema taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment