Wednesday, August 14, 2019









1972 ni mwaka ambao wazo la michuano ya Super Cup lilianzishwa na mashabiki wa England ambao walitaka kuona bingwa wa European Cup na Champion League ujumbe huo ulichapishwa kwenye moja ya gazeti Ulaya.

Hatimaye mwaka 1973 Super Cup ya kwanza ilichezwa, iliwashindanisha Mabingwa wa mwaka 1972 wa European League na Champion League ambao iliwakutanisha Ajax dhidi ya Rangers.

De Telegraaf, Anton Witkamp hawa walilikazania wazo hilo wakiwa ni waandishi na kushuhudia fainali ya kibabe kati ya Ajax akiibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 6-3 dhidi ya Rangers.

Leo ni fainali ya Super Cup ambapo Liverpool itamenyana na Chelsea.

Jurgen Klopp Meneja wa Liverpool amesema: " Ni kombe gumu na ushindani ni mkubwa, kuhusu kushinda ni fainali yenyewe itaamua, ila mwaka huu nitakuwa tofauti kidogo,". 


Meneja wa Chelsea, Frank Lampard alitupia jumla ya mabao 7 walipokutana na Liverpool kwenye mechi 39 Leo anaongoza kikosi chake kumenyana na Liverpool.

"Kuna mengi ya kufanya nina amini utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari,".

Mchezo wa leo ulimwengu utashuhudia mwanamke akiwa refa wa kati kwenye mchezo mgumu na mkubwa wa mashindano haya ambaye ni France Stephanie amesema kuwa hana hofu yoyote kwake ni kawaida.

0 comments:

Post a Comment