Saturday, August 24, 2019



Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta akiwa na club yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji dhidi ya Anderletch katika uwanja wa Luminus.
Samatta ameonesha makali yake baada ya kufanikisha ushindi wa goli 1-0 alilolifunga dakika ya 54 kwa assist nzuri kutoka kwa Junya Ito na kuzibakisha point tatu nyumbani.
Uwepo wa mastaa waliowahi kucheza katika Ligi Kuu England kama Samir Nasri na Vincent Kompany wameshindwa kuisaidia timu ipate ushindi wake wa kwanza msimu huu, hiko ni kipigo cha tatu cha Anderletch msimu huu kati ya michezo mitano na akipata sare mbili.

0 comments:

Post a Comment