Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema hakuna timu yoyote itakayoruhusiwa kubadili rangi ya nembo ya mdhamini katika jezi.
Kauli hiyo imekuja kufuatia sintofahamu ya nembo ya mdhamini mkuu ambaye ni Vodacom na Yanga kubadilishwa misimu kadhaa nyuma na kuwa ya kijani.
mambo yameonekaka kuwa tofauti kwa msimu huu na sasa rangi ambayo itatumika kwa timu zote itasalia kuwa ileile nyekundu.
Karia amesema hatua za kisheria kwa atakayebadili rangi ya mdhamini zitachukuliwa.
"Mkataba wetu wa udhamini una masharti yake ambayo tunatakiwa kuyafuata na hatutoruhusu yeyote kwenda kinyume nayo.
"Masharti hayo ni kama kitabu cha msahafu na kila mmoja anapaswa kuyafuata. Yeyote ambaye hatoyafuata tutamtoa kwenye familia yetu," amesema Karia.
0 comments:
Post a Comment