Saturday, August 24, 2019



Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali ya mchezaji huyo kujeruhiwa mara kwa mara. (Marca – in Spanish). Lakini ripoti zinaarifu kuwa Real na mahsimu wao Barcelona wanahoji masharti ya malipo ya hali ya juu yanayodaiwa na Neymar. (AS – Spanish)

Baba mzazi wa na wakala wa beki wa Arsenal wa miaka 27-Shkodran Mustafi wanasema mchezaji huyo raia wa Ujerumani ana mpango wa kuhama klabu hiyo. (Mirror)
Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 28, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya na klabu hiyo ambayo itaongeza mara mbili malipo ya mchezaji huto wa raia wa Uholanzi hadi £250,000 kwa wiki. (90min)
Alexis SanchezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Chile, Alexis Sanchez
Manchester United wana matumaini ya kumuuza mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30, kabla dirisha la usajili wa wachezaji barani ulaya kufungwa. (Mirror)
Wachezaji wa United wanataka mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 21, awe akipiga mikwaju ya penalti baada ya mkwaju wa penalti wa Paul Pogba kushikwa wakati wa mechi yao dhidi ya Wolves. (Mail)
Tottenham wanatafakari kumuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, wakipokea dau la angalau £50m. (Mail)
Christian EriksenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDenmark Christian Eriksen, Kiungo wa kati wa Tottenham
Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane, 23, huenda akarejea uwanjani msimu huu baada ya kuumia goti wakati wa michuano ya Community Shield mapema mwezi Agosti. (Sun)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane haamini kipa wake Keylor Navas, 32, ataondoka klabu hiyo licha ya tetesi zinazomhusisha na Paris St-Germain.(Marca)
Bayern Munich wanajiandaa kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Ureno Renato Sanches,aliyejinga na Lille, kiungo wa kati wa Espanyol Mhispania Marc Roca anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (L’Equipe – in French)

0 comments:

Post a Comment