Inter Milan
imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu kiungo wa Chile Alexis
Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, na wanataka kukamilisha mkataba wa
mkopo katika siku tatu zijazo. (Mirror)
Barcelona imewasilisha
ombi jipya kwa mshambuliaji wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain na
wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka 27,
linalojumuisha "fedha zaidi na wachezaji zaidi". (Telefoot )Tottenham inahofia itampoteza mchezaji wa kiungo cha kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, fkwa kitita kidogo cha £30m kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Star)
- Man City yawika Newcastle yailaza Tottenham
- Simba yaaga mashindano ya ligi ya mabingwa Caf
- David Rudisha apata ajali mbaya ya barabarani

Norwich itamfukuzia kipa wa Stoke na timu ya taifa ya England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari na iwapo thamani yake itashuka. (Sun)
Bordeaux inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na Misri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, kwenda Ligue 1 kwa mkopo. (Foot Mercato)
Leeds inatarajiwa kuanza mara moja mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati Kalvin Phillips kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo wa miaka 23 anataka kulipwa £40,000 kwa wiki ili kuendelea kusalia Elland Road. (Football Insider)
Aliyekuwa beki kamili wa Chelsea Filipe Luis, mwenye umri wa miaka 34, amekataa ombi la Manchester City, Lyon na Borussia Dortmund msimu huu wa joto kabla ya kujiunga na Flamengo kutoka nchini anakotoka Brazil. (Globo Esporte)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemkaribisha mchezaji wa kiungo cha kati wa Exeter Ben Chrisene kufanya mazoezi na klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka timu ya vijana wa timu ya taifa England alifanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza mwezi huu. (Sun)
TETESI ZA JUMAPILI
Watford inafikiria hatma ya mkufunzi wake Javi Gracia baada ya kuanza kampeni yao ya Premia baada ya kupoteza mara tatu na hivyobasi kushindwa mara saba mfululizo kutoka msimu uliopita.. (Mail on Sunday)Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kipa wa Everton mwenye umri wa miaka 36 Maarten Stekelenburg iwapo mlinda lango wao raia wa Chile Keylor Navas, 32, atahamia PSG. (Football Insider)
- Ubaguzi dhidi ya Pogba wazua hisia kali
- Pogba akosa penalti huku Man United ikizuiwa na Wolvehampton
- 'Acheni kusambaza chuki mtandaoni' - Solskjaer

Tottenham wana matumaini kwamba beki wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 Toby Alderweireld atatia kandarasi mpya . (Sun on Sunday)
Fiorentina imejiunga katika harakati za kumsaini mshambuliaji wa Liverpool na Enlgand Bobby Duncan kwa mkataba wa msimu huu . (Mail on Sunday)
Southampton inamchunguza mshambuliaji wa QPR mwenye umri wa miaka 21 Eberechi Eze kabla ya uhamisho wa mwezi Januari . (Sun on Sunday)
Sampdoria ina hamu ya kumsaini kipa wa Aston Villa na Croatia Lovre Kalinic, 29. (Il Secolo XIX - in Italian)
Fifa inachunguza iwapo Roboti zinaweza kuchukua mahala pao marefa wa usaidizi ili kutoa maamuzi ya mipira ya kuotea kwa kuwa tayari wanasaidia katika VAR. (Sunday Mirror)

0 comments:
Post a Comment