Tuesday, October 22, 2019


Kiungo wa timu ya taifa ya Uswis na klabu ya Arsenal, Granit Xhaka amemtolea uvivu beki wa zamani wa Manechester United, Patrice Evra baada ya kuonyesha dharau juu ya washika bunduki hao wa London na kumwambia anapaswa kuwa makini na anachozungumza.
Midfielder Granit Xhaka has hit back at Patrice Evra for calling Arsenal's players 'babies'
Xhaka amesema ”Nina mheshimu sana kwasabu ni mchezaji bora, lakini anapaswa kuwa makini kwa kile anachozungumza. Anafahamu hali ilivyo kwa sasa, lakini siyo yeye tu wapo wengine wengi wanaosema vibaya.” amesema mchezaji huyo.

Patrice Evra amevunja ukimya na kuamua kufunguka mtazamo wake juu ya klabu ya Arsenal na kusema kuwa kikosi chao ni dhaifu na ndiyo maana siku zote yeye amekuwa akiwaita watoto, hii inajiri baada ya washika bunduki hao wa London kukubali kipigo cha bao 1 – 0 dhidi ya Sheffield United.
Patrice Evra walks out through a guard of honour from Arsenal following Manchester United's 2012/13 Premier League title win
Kikosi cha ‘The Gunners’ kilikuwa ugenini na kulazimika kipigo hicho ambacho kimewafanya kushindwa kuwa kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa Premier League, baada ya Lys Mousset kutupia bao dakika ya 30 na kuipatia timu ya Sheffield United pointi tatu usiku huo.
Evra, ambaye alikuwa mgeni kwenye MNF, amefunguka na kusema kuwa Arsenal  siku zote amekuwa akiwaita ‘Watoto’ wakati akiwa Manchester United na bado anaamini timu hiyo bado haija badilika tangu alivyoondoka kocha Mzee Arsene Wenger.
Evra told Robin van Persie he had joined a 'man's club' following his move to Manchester United from Arsenal
“Sheffield United walistahili ushindi, lakini pia sikushangazwa na kipigo hicho kwa Arsenal,” Evra ameiyambia Monday Night Football (MNF).
Patrice Evra ameongeza “Kwa miaka 10 nimekuwa nikiwaita Arsenal watoto, na bado wapo hivyo, pindi ninapo waangalia naona kama wanangu na huo ndiyo ukweli na kusema hivyo wala sio kwamba nimewakosea heshima.”

“Wanaonekana wapo vizuri, lakini hawaonekani kama timu ya ushindi. Wanacheza mpira mzuri, lakini nilikuwa mwenye furaha kubwa pindi nilipokuwa nikicheza nao kwasababu nilikuwa nafahamu mchezo huo tunakwenda kushinda.”

“Na hata Robin van Persie alivyotua Manchester, siku ya kwanza kabisa nilimshika mkono na kumwambia karibu katika timu ya wanaume. Mwanzoni hakufurahishwa na kauli yangu, lakini baada ya mwezi mmoja aliniambia, Patrice ulichoniambia ulikuwa sahihi.”

“Wana wachezaji wakubwa David Luiz, Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, lakini bado kuna kitu kinamisi kwa miaka kadhaa sasa.”

“Na waheshimu mno Aubameyang na Lacazette, lakini kama hawa wawili hawatakuwa wakifunga magoli, basi watakuwa kwenye matatizo na hakuna kitakachobadilika, yupo wapi leo hii kocha, Arsene ?’ ilikuwa hivyo hivyo.”

0 comments:

Post a Comment