Samatta ambaye ni Mtanzania pekee aliyepata bahati ya kucheza michuano hiyo mikubwa kabisa barani Ulaya, anatarajiwa kushuka uwanjani huku akiwa na jezi yake ya rangi ya Blue ikiashiria kuwa wapo nyumbani na klabu yake ya KRC Genk huku akiwapatia furaha watazamaji watakao kuwa wanaufuatilia mchezo huo.
Katika kuelekea mchezo huo mshambuliaji huyo amezungumza na vyombo vya habari na kuweka wazi malengo yao kama timu huku akisema kuwa Watazania hivi sasa wanauzungumzia mechi hiyo ya kesho, wakimzungumzia yeye dhidi ya beki bora kwa sasa duniani (Virgil) Van Dijk, huku wakimtaka afanye kitu.
”Wakati
nilipokuwa mdogo nilikuwa nikiishabikia Manchester United, lakini kwa
sasa hatuzungumzii Manchester United bali ni Liverpool,” amesema
Samatta.
”Tunaamini Liverpool ni timu
imara kwa sasa katika Premier League na hata kwenye michuano ya
European, hivyo tunatarajia mchezo utakuwa mgumu. Tunacheza mbele ya
mashabiki wetu hivyo tunahitaji tuwe wenye furaha mwishoni mwa mchezo.
Hivyo tutafanya kwa uwezo wetu wote.”
”Nchini
Tanzania, kila mmoja atakuwa anaufatilia huo mchezo wa kesho,
wananizungumzia mimi na Van Dijk. Wanasema nilazima nifanye kitu dhidi
yake, niende mbele yake, ni ‘dribble’, nafikiria mambo mengi sana juu
yao.”
0 comments:
Post a Comment